BurudaniMilele FmSwahili

Kanye West Kuwania urais Marekani mwaka wa 2020

Mwanarapa Kanye West ametangaza azma ya kuwania Urais wa Amerika katika kipindi cha miaka mitano.

Mwanarapa huyo wa miaka 38  maarufu kwa vibao kama Heartless, Gold Digger na FourFive Seconds aliitumia jukwaa la tuzo za MTV Awards hapo siku ya Jumapili kutangaza nia yake ambayo iwapo itafaulu itamfanya kuwa Rais wa pili mweusi kuwahi shikilia hatamu nchini humo.
Tangazo hilo lilijiri baada ya mwanarepa huyo kupewa tuzo la mafanikio ya ufanisi katika taaluma yake ya takriban miaka 19 katika ulingo wa muziki.

“Nimeafikia uamuzi wa kuwania urais katika uchaguzi wa 2020,” alisema huku akikiri kutumia bangi kabla ya kupanda jukwaa hilo ambapo tangazo lake lilipokelewa na shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki vile vile mkewe, Kim Kardashian anayetarajiwa kujifungua mtoto wao wa pili mwisho wa mwaka huu.

Kanye na mkewe Kim Kardashian
Kanye na mkewe Kim Kardashian
Kanye na mkewe Kim Kardashian
Kanye na mkewe Kim Kardashian
Kanye West, Kim Kardashian, Kourtney Kardashian, Kris Jenner and Kylie Jenner
Kanye West, Kim Kardashian, Kourtney Kardashian, Kris Jenner na Kylie Jenner
Show More

Related Articles