HabariMilele FmSwahili

Josephine Kabura na washukiwa wengine 10 wa sakata ya NYS wafunguliwa upya mashtaka ya ufujaji wa shillingi milioni 791

Mwanabiashara Josephine Kabura na washukiwa wengine kumi wa skata ya ufujaji wa fedha katika shirika la NYS wamekana mashtaka mapya kumi na sita ya ufujaji wa shilingi milioni 791.

Mbele ya hakimu mkaazi wa mahakama ya Milimani Martha Mutuku Kabura na wenzake wamekana kutumia visivyo fedha za NYS katika ununuzi wa mali sawa na magari mwaka 2015.

Kabura,mwanabiashara Ben Gethi Wangui, John Kago Ndungu,Patrick Ogolla Onyango wanadaiwa kushirikiana kununua gari aina ya Range Rover yenye sajili ya KCB 750z yenye thamani ya shilingi milioni 23 kati ya Disemba 31 mwaka 2014 na Aprili 30 mwka 2015,fedha zinazodaiwa kufujwa katika shirika hilo.

Wakati uo huo Kabura,Kago na mamake Gethi Charity Wangui Gethi wanadaiwa kupanga njama ya kununua gari aina ya Jeep Cherokee yenye usaliji KCD 241q yenye thamani ya shilingi milioni 6.3

Show More

Related Articles