HabariMilele FmSwahili

Jaji mkuu Maraga abuni jopo la majaji 3 kuamua kesi ya kupinga wabunge kujitengea marupurupu ya nyumba

Jaji mkuu David Maraga amebuni jopo la majaji watatu kuskiza na kuamua kesi inayopinga hatua ya wabunge kujitengea bajeti ya kugharamikia marupurupu ya makaazi. Watatu hao ambao wataongozwa na jaji Pauline Nyamweya, Eeldon Korir na jaji John Mativo wataskiza na kuamua kesi hiyo ambapo wabunge wamejitengea shilingi elfu 250 kila mwaji ezi za makaazi tangu mwezi Oktoba mwaka jana

Jopo hilo limebuniwa kufuatia ombi la jaji Weldon Korir wa mahakama kuu anayesema masuala yanayohusishwa katika kesi hiyo yanaibua utata wa sheria na kuwa yanahitaji majaji kushauriana

Show More

Related Articles