HabariMilele FmSwahili

Vikao vya kumhoji Jaji Jackton Ojwang kuanza mwezi ujao

Vikao vya kumhoji jaji wa mahakama ya juu aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma za utovu wa nidhamu Jackton Ojwang, vitaandaliwa mwezi ujao. Idara ya mahakama imedhibitisha kuwa jopo lililoteuliwa kuchunguza madai yanayomwandamana jaji Ojwang litaandaa vikao vyake faraghani tarehe 15 Julai. Ni kufuatia ombi la Jaji Ojwang kuwa vikao hivyo viandaliwe faraghani. Jaji Ojwang alisimamishwa kazi na rais Uhuru Kenyatta mwezi Aprili mwaka huu. Tume ya JSC ilipendekezwa kusimamishwa kazi kwake baada ya kupokea malalamishi kuhusiana na madai kuwa alisikiliza na kutoa maamuzi ya upendeleo wa baadhi ya kesi. Malalamishi hayo yaliwasilishwa na Nelson Oduor Onyango

Show More

Related Articles