HabariMilele FmSwahili

IPSOS : 44% ya wakenya wataka huduma za afya kusimamiwa na serikali kuu

Asilimia 44 ya wakenya wanataka huduma za afya kusimamiwa na serikali kuu badala ya serikali za kaunti ilivyo wakati huu. Utafiti wa shirika la IPSOS unaonyesha ni asilimia 36 pekee ya wakenya wanaotaka sekta hiyo kubaki kwa serikali za kaunti. Akitoa ripoti ya utafiti huo, mtafiti mkuu wa IPSOS Tom Wolf anasema asilimia 84 ya wakenya wanaunga mkono mfumo wa ugatuzi,hii ikijumuisha asilimia 86 wafuasi wa Jubilee na asilimia 83 wafuasi wa NASA. Vile vile,asilimia 27 ya wakenya wanataka magavana kuangazia kuboresha barabara ambazo ziko katika hali mbaya kama njia ya kuimarisha uchumi.

Show More

Related Articles