HabariMilele FmSwahili

IEBC, tayari kwa chaguzi ndogo za kesho

Tume ya uchaguzi IEBC inaendelea na matayarisho ya chaguzi ndogo ya ubunge Baringo Kusini na zile za wadi za Bobasi Chache na North Kadem zitakazoandaliwa kesho. Katika eneo la Baringo Kusini wakazi watamchagua mbunge mpya kumrithi Grace Kipchoim aliyefariki akipokea matibabu katika hospitali moja hapa jijini Nairobi mwezi aprili.Kwengineko wagombeaji 10 watakabiliana katika uchaguzi mdogo wa wadi ya Bobasi Chache kaunti ya Kisii. Uchaguzi huo unafuatia agizo la mahakama ya Ogembo iliyofutilia mbali ushindi wa Fred Sambu’s kwa madai uchaguzi agosti saba haukuwa huru.Na katika kaunti ya Migori wagombeaji wawili wawanania kiti cha mwakilishi wadi ya North Kadem kufuatia kifo cha aliyekuwa mwakilishi Boaz Okoth mapema mwaka huu.

Show More

Related Articles