HabariMilele FmSwahili

Idadi ya waliofariki kufuatia ajali eneo la Kilimambogo yafikia watu 17

Idadi ya waliofariki baada ya matatu kugongana na lori katika eneo la Kilimambogo imefika watu 17. Watu 10 akiwemo dereva wa matatu walifariki papo hapo huku wengine wakiaga hospitalini. Aidha mmoja kati ya tisa waliojeruhiwa anaarifiwa kuwa hali mahututi katika hospitali ya Thika level 5. Kulingana na polisi matatu ya shirika la Kinatwa Sacco ilikuwa ikielekea Kitui kutoka Nairobi ilikuwa ikijaribu kupita magari mengine ilipogongana ana kwa ana na lori hilo. Yakijiri hayo watu 26 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani baada ya basi la shule ya upili ya Queen of Peace High School, Ruriuni kugongana na gari dogo aina ya Toyota Noah katika eneo la kibunjia. Mtu mmoja ameripotiwa kuwa hali mahututi. Kwengineko watu wanane wamejeruhiwa kufautai ajali ya matatu na basi katika eneo la Molo barabara ya Nakuru Eldoret

Show More

Related Articles