HabariMilele FmSwahili

Huduma za afya zatatizika kaunti ya Kisumu baada ya wahudumu wa afya kugoma

Huduma za afya zinatatizika katika hospitali za umma kaunti ya Kisumu kufuatia mgomo wa wahudumu wa afya kaunti hiyo. Naibu katibu mkuu wa KNUN Maurice Opetu ameisuta serikali ya gavana Peter Anyang Nyongo kwa kufeli kuangazia matakwa yao.

Wahudumu hao wa afya akiwemo wanaojumuisha wauguzi,maafisa wa kliniki,KMPDU na wale wa maabara wameapa kutorejea kazini kamwe hadi pale lalama zao zitakapoangaziwa.

Baadhi ya maswala wanayoyataka kuangaziwa ni pamoja na kulipwa mishahara yao ya miezi mitatu,kupandishwa vyeo na kulipa ada zao za NHIF.

Show More

Related Articles