Milele FmSwahili

Hofu yatanda Kericho kuhusiana na ugonjwa wa Ebola

Idara ya afya kaunti ya Kericho imewekwa katika tahadhari ya hali ya juu kufuatia kutengwa mgonjwa mwanamke aliyeripotiwa kudhihirisha dalili za homa hatari ya Ebola. Kisa hiki kimeripotiwa kwenye hospitali ya rufaa mjini Kericho ambapo mgonjwa huyo alifika usiku wa kuamkia leo kusaka matibabu baada ya kuwasili kutoka mji wa mpakani wa Malaba alikokuwa amekutana na mumewe. Kulingana na afisa wa mawasiliano katika hospitali hiyo Timothy Kimei, chembe chembe za damu za mgonjwa huyo kwa sasa zinafanyiwa ukaguzi katika maabara ya shirika la utafiti wa dawa KEMRI kubaini maradi anayougua. Kemei amesema matokeo ya utafiti huo yatatolewa leo huku akiwataka wakazi wa Kericho kusalia watulivu

Show More

Related Articles