HabariMilele FmSwahili

Hassan Wario na Harun Komen waachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1

Balozi wa Kenya nchini Austria Hassan Wario pamoja na Harun Komen wamechiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1. Hii ni baada yao kukanusha mashtaka 6 ya kuhusika katika uharibifu wa shilingi milioni 55  zilizotengewa kikosi cha Kenya kilichoshiriki mbio za olimpiki za Rio nchini Brazil mwaka wa 2016. Hakimu mkuu wa mahakama ya ufisadi Douglas Ogoti ameagiza kikao cha kupanga kesi yao kuandaliwa tarehe 16 Novemba.Ombi la Wario kurejeshewa pasi yake ya usafiri hata hivyo limekataliwa  huku ofisi ya kiongozi wa mashtaka kwa ushurikiano na wizara ya mambo ya kigeni zikitarajiwa kutoa mwelekeo. Aidha upande wa mashtaka umedokeza nia ya kupinga ombi hilo.

Show More

Related Articles