HabariMilele FmSwahili

Hakimu Brian Khaemba ajiuzulu

Hakimu Brian Khaemba sasa anasema amejiuzulu baada ya kubaini hatapokea mshahara katika muda aliosimamishwa kazi. Katika barua kwa tume ya huduma za mahakama JSC, Khaemba anasema kando na kujiuzulu kama hakimu wa mahakama ya Kiambu,pia amejiuzulu kama katibu mkuu wa chama cha majaji na mahakimu(KJMA). Anasema hatua hiyo itamwezesha kusaka mbinu mbadala za kupata pato lake la kila siku. Khaemba alisimamishwa kazi na jaji mkuu David Maraga baada ya kupatikana na hatia ya kuidhinisha dhamana ya kuzuia kukamatwa kwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu na makachero wa tume ya EACC mwezi uliopita.

Show More

Related Articles