MichezoMilele FmSwahili

Gor Mahia yaporwa Algeria

Matumaini ya klabu ya Gor Mahia ya kufika katika hatua ya robo fainali katika michezo ya mashirikisho barani Afraka yalipata pigo jana usiku hii ni baada ya kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Hussein Dey ya Algeria.Goli la pekee la Hussein lilitiwa nyavuna na Abderehmanne Yousfi dakika ya 9.

Hata hivyo mwamuzi wa mechi hiyo Boubou Traore kutoka Mali amekashifiwa pakubwa kwa kutupilia mbali goli la wazi la Kogallo kipindi cha pili.Vijana hao wa Kenya wanaondoka Algeria adhuhuri kulekea Misri ambako watacheza na wenyeji Zamalek jumapili ijayo.

Katika matokeo mengine ya kundi D ni kwamba Petro Atletico iliambulia kichapo cha 1-0 dhidi ya Zamalek mjini Luanda na kufanya kundi hilo kuwa wazi.

Hadi kufikia sasa baada ya mechi nne,Hussein Dey ipo kidedea kwa alama saba ikifuatwa na Gor Mahia ilio ya pili kwa alama sita.Zamalek imejifufua kundini ikiwa ya tatu kwa alama tano wakati Petro ikishika mkia kwa alama 4.

Show More

Related Articles