HabariMilele FmSwahili

Godfrey Osotsi aondolewa kwenye sajili ya chama cha ANC

Mbunge maalum wa chama cha ANC Godfrey Osotsi huenda akapoteza  kiti chake baada ya jina lake kuondolewa kwenye sajili ya  chama hicho. Uongozi wa ANC kupitia katibu wake Barack Muluka ulimwandikia msajili wa vyama kutaka jina lake Osotsi kuondolewa kwenye sajili  ya chama. Ni barua ambayo msajili wa vyama  Anne Nderitu  amekiri kupokea barua hiyo na kuondoa jina  la Osotsi.

Show More

Related Articles