HabariMilele FmSwahili

Gavana Obado akana kuhusika na mauaji ya Sharon Otieno

Gavana wa Migori Okoth Obado amekana kuhusika na mauaji ya mwanafunzi wa chuo cha Rongo Sharon Otieno.Akizungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza tangu kutuhumiwa na mauaji hayo,Obado amesema yuko tayari kujitetea mahakamani.Obado ambaye alikuwa ameambatana na familia yake, amesema waliohusika wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria. Amelalamikia kuhusishwa na mauaji hayo akisema ameomba vyombo vya usalama vinapaswa kupewa nafasi ya kuendesha uchunguzi na kutendea haki familia ya Sharon.Obado amezungumza saa chache baada ya jaji wa mahakama ya Milimani Luka Kimaru kuagiza msaidizi wake, Micheal Oyamo kusalia rumande kwa siku 14.hatua hii inalenga kuipa upande wa mashtaka muda wa kukamilisha uchunguzi kuhusiana na mauaji ya Sharon.Kesi hiyo itarejelewa tarehe 26.

Show More

Related Articles