HabariMilele FmSwahili

Gavana Obado aachwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5

Gavana wa Migori amepata afueni baada ya mahakama kuu kumwachilia jwa dhamana kuhusiana na kesi ya mauaji ya Sharon Otieno. Jaji wa mahakama kuu Jessi Lessit ametoa uamuzi wa kuachiliwa huru kwa Obado kwa dhamani ya shilingi milioni 5 na wadhamini wawili wa kiasi sawa. Kadhalika Gavana Obado ameagizwa kusalimisha pasi zake za usafiri, kuonywa dhidi ya kuwasiliana na mashahidi katika kesi hii.Kadhalika ameonywa dhidi ya kuwatishia familia ya Sharon Otieno. Hata hivyo jaji Lessit amekataa ombi la msaidizi wake Micheal Oyamo na karani wa bunge la Migori Caspel Obiero kwa misingi kuwa huenda wakavuruga uchunguzi wa kesi hiyo.

Show More

Related Articles