HabariMilele FmSwahili

Gavana Muriithi atishia kuwafuta madaktari wanaogoma kaunti ya Laikipia

Gavana wa Laikipia Ndiritu Muriithi amewaagiza madaktari wanaogoma kwa juma la pili sasa kurejea kazini lau sivyo watimuliwe. Gavana Murithi amewasuta madkaktari hao kwa kupuuza maslahi ya wagonjwa na kushiriki mgomo ulioharamishwa na mahakama. Kadhalika amepinga shinikizo lao kuongezewa mishahara akidai kwa sasa wanapokea mshahara wa juu.

Akizungumzia swala la kucheleweshwa kwa mishahara ya wafanyakazi wa kaunti Ndiritu ameelekeza kidole cha lawama kwa wizara ya fedha kuwa inachelewa kwa kuwapa fedha.

Show More

Related Articles