HabariMilele FmSwahili

Dennis Itumbi aachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja

Mahakama imemwachilia kwa dhamana ya shilingi laki moja mkurugenzi wa mawasiliano katika afisi ya naibu rais Dennis Itumbi katika kesi ya kusaka muasisi wa waraka ulio ibua njama ya kuwawa naibu rais William Ruto. Jaji wa mahakama hiyo Zainab Abdul ameafikia hatua hiyo baada ya kupuuzilia mbali pendekezo la upande wa mashtaka uliotaka Itumbi kuzuiliwa kwa siku tisa zaidi kufanikisha uchunguzi. Jaji Abdul anasema vigezo vinavyotumika na upande wa mashtaka kutaka kumzuilia Itumbi kwa siku hizo Havina uzito wa kutosha. Wakati uo huo mahakama imetoa masharti kadhaa kwa Itumbi ikiwemo kujisalimisha kwa DCI mara moja kila baada ya siku mbili kwa siku tisa zijazo.

Nao viongozi wafuasi wa naibu rais William Ruto waliokuwa mahakamani wakati wa kutolewa uamuzi huo, wameitaka mahakama kumruhusu Itumbi kuwasilisha kanda ya video inayosema inadhibitisha madai yake. Wakiongozwa na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa, wabunge hao wanasema hawatoiruhusu mahakama hiyo kuwapotosha wakenya.

Ichungwa amekiri  kuwa mwanachama wa kundi la whatsapp linaloibua utata katika madai hayo na kusema yuko tayari kuandikisha taarifa na idara ya upelelezi nchini DCI

Show More

Related Articles