HabariMilele FmSwahili

Deni la taifa huenda likafika shilingi trilioni 7 mwaka wa 2022

Deni la taifa huenda likafikia shilingi trilioni 7, mwaka wa 2022, wakati rais Uhuru Kenyatta akikamilisha kuipindi chake.Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya usimamizi wa madeni iliyowasilishwa bungeni hapo jana.Ripoti hii iliyoandaliwa na wizara ya fedha inaashiria kwa sasa Kenya inadaiwa shilingi trilioni 5.1 kufikia Juni mwaka huu.Uchina ndio mkopeshaji mkubwa zaidi wa kenya ikiidai shilingi bilioni 559.1, Italia inafuata kwa shilingi bilioni 101.9, Ujerumani bilioni 34.7, Uubelgiji bilioni 10.2 na Marekani bilioni 2.9.Ripoti hii inawadia wakati viongozi wa kisiasa wakimtaka rais Kenyatta kusaka mbinu za kubadili hali hii.  .Hata hivyo naibu rais William Ruto ametetea serikali akisema fedha zinazokopwa zitalipwa kwa wakati kwani miradi inayoendeshwa itafanikisha kulipa mikopo hiyo, anavyoeleza naibu wa rais William Ruto.

Show More

Related Articles