HabariMilele FmSwahili

Chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret chafungwa kwa muda usiojulikana

Chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret kimefungwa kwa muda usiojulikana. Hii ni baada ya wanafunzi kukabiliana na maafisa wa polisi katika maandamano ya kupinga kuongezwa kwa pesa za mtihani sawa na kutaka kuajiriwa wahadhiri zaidi.

Kiongozi wa wanafunzi Idda Harrison amejeruhiwa vibaya katika maandamano hayo.

Aidha wanafunzi hao wamewashtumu maafisa wa polisi kwa kutumia risasi kuwakabili wakimtaka waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi kuchunguza madai hayo.

Show More

Related Articles