HabariMilele FmSwahili

Chuo cha Masinde Muliro chafungwa baada ya wanafunzi kuandamana mapema leo

Chuo cha Masinde Muliro kimefungwa  baada ya wanafunzi kushiriki maandamano na kufunga barabara ya Kakamega –Webuye kulalamikia kile wanachodai ni uongozi mbaya chuoni humo. Wanafunzi wamepewa hadi saa nane kuondoka katika majengo ya chuo hicho

Wanafunzi hao wanalalamikia huduma mbovu ya mtandao chuoni humo sawa na kutakiwa kumaliza karo kabla ya kufanya mtihani. Imewalazimu maafisa wa polisi kutumia vitoa machozi kuwatawanya wanafunzi hao.

Maandamano sawia yameshuhudiwa katika chuo cha kiufundi cha TUM mjini Mombasa. Tayari zaidi ya wanafunzi 20 wa chuo hicho wametiwa mbaroni na maafisa wa polisi baada ya kuandamana na kufunga barabara eneo la Buxton. Wanafunzi hao walikuwa wanalalamikia uongozi mbaya chuoni humo.

Show More

Related Articles