HabariMilele FmSwahili

Tob Cohen kuzikwa Jumatatu ijayo katika makaburi ya Wayahudi Nairobi

Bwenyenye Tob Cohen atazikwa Jumatatu ijayo katika makaburi ya Wayahudi hapa Nairobi. Ni baada ya mkewe Cohen, Sarah Wairimu, na dadake Cohen, Gabrielle Van Straten kushauriana na mawakili wao na kupata muafaka.
Mazishi hayo aidha yatahudhuria na familia pekee. Wakili Cliff Ombeta anayemwakilisha dadake Cohen, Gabriella Cohen na Philip Murgor anayemwakilisha Sarah Wairimu mkewe Cohen wanasema wateja wao wamekubaliana kushiriki pamoja mazishi hayo ili kuzuia mvurutano wa mwili wa Cohen.
Wakati uo huo mawakili hao wamedokeza tayari matokeo ya upasuaji wa mwili wa Cohen yametoka japo wanasema sio wajibu wao kuelezea umma jinsi Cohen alifariki.

Show More

Related Articles