HabariMilele FmSwahili

Bunge kurejelea vikao vyake leo

Bunge linarejelewa vikao vyake leo baada ya mapumziko ya juma moja. Aidha wabunge wanakabiliwa na vibarua kadhaa ikiwemo kuchaguliwa kwa mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu bajeti sawa na kufanyiwa mabadiliko kamati hiyo. Duru za kuaminika zinaarifu kuwa upande wa JUBILEE unataka kupigia debe kusalia afisini kwa mwenyekiti wa sasa Mutava Musyimi. Aidha vute ni kuvute inatarajiwa kati ya wabunge wanaoegemea upande wa JUBILEE na ule wa CORD huku wale wa CORD wakiahidi kutokubali kurejeshwa afisini kwa Mutava Musyimi. Hii itakuwa mara ya tatu kwa wabunge kujaribu kufanyia marekebisho uongozi wa kamati hiyo.

Show More

Related Articles