HabariMilele FmSwahili

Bendera ya Kenya kupepea nusu mlingoti, asema Rais Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza kupeperushwa kwa bendera nusu mlingoti kuanzia hapo kesho Jumamosi hadi Jumatatu kama njia moja ya kumwomboleza aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Katika taarifa, Rais Uhuru Kenyatta ametaja kifo cha Mugabe kama pigo kuu kwa taifa la Zimbabwe. Naibu Rais William Ruto amesema Mugabe atakumbukwa kwa mchango wake barani Afrika. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pia amepongeza mchango wa marehemu barani Afrika. Mugabe amefariki mapema leo nchini Singapore akiwa na miaka 95 takriban miaka miwili tangu kubanduliwa kwake madarakani.

Show More

Related Articles