MichezoMilele FmSwahili

Beki wa Harambee Stars ajiunga na klabu ya Sweden

Beki shupavu wa Harambee Stars Joseph ‘Crouch’ Okumu amejiunga na klabu IF Elfsborg ya Sweden kutoka Real Monarchs ya Marekani.

Okumu mwenye umri wa miaka 22, anaingia kupiga soka ya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya kusakatia Real Monarchs kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Beki huyo wa zamani wa klabu ya Chemilil Sugar ya Kenya na Free States Stars ya Afrika Kusini alikuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Harambee Stars kilichoshiriki fainali za taifa bingwa barani Afrika 2019 nchini Misri ambako alicheza mechi zote tatu za kundi cha C dhidi ya Aljeria,Tanzania na Senegal.

Okumu anajiunga na wachezaji wengine wa Harambee Stars Eric ‘Mercelo’ Ouma na Ovella Ochieng wanaopigia klabu ya Vasalunds IF nchini Sweden.

Show More

Related Articles