HabariMilele FmSwahili

Bei ya unga kupanda kutoka shilingi 75 hadi 100 kwa kila mfuko wa kilo 2

Kuanzia wiki ijayo bei ya unga wa mahindi itapanda kutoka shilingi 75 hadi 100 kwa kila mfuko wa kilo mbili.Muungano wa wasaga nafaka unasema nyongeza hiyo inatokana na ukosefu wa mahindi nchini. Mwenyekiti Peter Kuguru anasema walipoafikia na serikali kupunguza bei gunia moja la mahindi liliuzwa shilingi 1600 ila sasa gunia hilo linauzwa kwa shilingi 2300.Kuguru na wenzake sasa wanaitaka serikali kutoa mahindi yanayozuiliwa katika maghala ya NCPB ili kuruhusu usagaji unga.

Show More

Related Articles