Milele FmSwahili

Baadhi ya viongozi wa ODM wadokeza kuwa Odinga atawania urais 2022

Baadhi ya viongozi wa ODM wamedokeza kuwa kinara raila Odinga atawania urais katika uchaguzi mkuu wa 2022. Seneta wa Siaya James Orengo na mbunge wa jumuia ya Afrika mashariki Oburu Odinga wanasema Raila ana haki kikatiba kusaka fursa ya uongozi wa nchi. Oburu aidha amewasuta baadhi ya viongozi wanaokihama chama hicho na kuingia katika vyama vingine huku akiwataja kuwa wasaliti. Vilevile wamesema upinzani utahakikisha kuwa serikali kutimiza ahadi ilizotoa kwa wakenya wakati wa kampeni.

Show More

Related Articles