HabariMilele FmSwahili

Aliyekuwa mwanahabari Esther Arunga kubaini hatma ya kesi ya mauaji dhidi yake leo

Aliyekuwa mwanahabari humu nchini Esther Arunga anatarajiwa kubaini hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili leo hii. Hii ni baada ya Arunga anayeishi Australia siku ya Jumatatu kukiri mbele ya mahakama nchini humo kuwa aliwahadaa maafisa wa polisi kuhusu kilichosababisha kifo cha mwanawe .Arunga anasema mumewe Quincy Timberlake ndiye aliyemuua mwanao wa miaka mitatu kwa kumpiga tumboni akitumia kifaa butu.Huenda  akahukumiwa kifungo cha maisha haswa kwa kuhujumu uchunguzi kuhusu kesi ya mauaji

Show More

Related Articles