HabariMilele FmSwahili

Aliyekuwa mwakilishi wadi wa Isukha Kakamega Richard Muchesia auwa familia yake kisha kujitoa uhai Rongai kaunti ya Kajiado

Aliyekuwa mwakilishi wadi wa Isukha ya kati kaunti ya Kakamega Richard Muchesia amemuuwa mkewe na watoto kisha akajitoa uhai hapa Nairobi. MCA huyo wa zamani anadaiwa kutekeleza unyama huo eneo la Rongai kaunti ya Kajiado usiku wa kuamkia leo. Polisi wanashuku ametekeleza mauaji hayo kwa kutumia bunduki  kisha kujitoa uhai kwa kujipiga risasi. Hata hivyo  polisi wanasema hawakupata chochote kuelezea sababu za kufanya unyama huo. Aidha miili yao tayari imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha city hapa Nairobi.

Show More

Related Articles