HabariMilele FmSwahili

Aliyekuwa mbunge wa Makadara Reuben Ndolo awachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili

Aliyekuwa mbunge wa Makadara Reuben Ndolo ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili kufuatia tuhuma za kutishia kumuua mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Richland Properties Rashid Hamid.

Hayo ni baada ya Ndolo kukana mashtaka hayo mbele ya mahakamaa.

Ndolo na wenzake saba walikamatwa na makachero wa idara ya upelelezi DCI usiku wa kuamkia Jumapili katika mkahawa wa Bustani Gardens ulioko bababara ya Oledume hapa Nairobi kwa kutishia kumwangamiza mfanyibiashara huyo wanayeng’ang’ania kipande cha ardhi hapa Nairobi.

Waliokamatwa na Ndolo ni Daniel Otieno Juma,George Otieno, Cyrus Nyamboga, Bernard Ochieng, Dick Otieno na Hassan Wario.

Show More

Related Articles