MichezoMilele FmSwahili

Algeria na Senegal kupambana katika fainali za AFCON 2019

Fainali ya kipute cha taifa bingwa barani Afrika itahusisha timu ya Senegal na Algeria hii ni baada ya timu hizo kusajili ushindi katika michuano ya nusu fainali jana usiku.

Algeria maarufu Kwama Mbweha wa jangwani imesajili ushindi wa 2-1 dhidid ya Nigeria na kuandikisha historia ya kufuzu kwa fainali ya afcon kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 29.

Beki wa Super Eagles Troost Ekong alijifunga na kuipatia Algeria uongozi dakika ya 40.

Odion Ighalo alisawazishia Nigeria kupitia kwa mkwaju wa panalti dakika ya 72.

Nyota wa Manchester City Riyad Mahrez alicheka na nyavu dakika ya 90 kupitia mkwaju maridada wa ikabu na kuiweka Algeria kwenye fainali.

 

Aljeria sasa itamenyana na Senegali iliocharaza Tunisia 1-0 katika nusu fainali ya kwanza.

Huyu hapa ni Mahrez kuhusu mchezo wa jana na fainali dhidi ya simaba wa Teranga Ijumaa ijayo.

Nyota wa Liverpool Sadio Mane ametaja fainali hiyo kuwa ngumu ila ameahidi kupambana kama timu kupata taji lao la kwanza la michuano hiyo.

Show More

Related Articles