HabariMilele FmSwahili

Ahmed Kolosh wa Jubilee ashinda kiti cha ubunge Wajir Magharibi

Mgombeaji wa Jubilee Ahmed Kolosh amenyakua ushindi  katika kinyanganyiro cha ubunge eneo la Wajir Magharibi. Afisa msimamizi wa uchaguzi huo Maurice Raria amemtangaza Kolosh mshindi kwa kura 11053. Ibrahim Sheikh wa KANU ameibuka wa pili kwa kura 6532. Matokeo hayo ni ya vituo vyote 75 vya upigaji kura. Jumla ya wapiga kura 17 606 walishiriki uchaguzi huo kati ya wote 27 544 waliosajiliwa.

Kolosh amewapongeza wapiga kura kwa kumuunga mkono huku akitoa hakikisho la kuwaunganisha wananchi eneo hilo

Ibrahim Sheik wa KANU amekiri kushindwa na kuapa kushirikiana na Koloshi kuwahudumia wananchi.

Show More

Related Articles