HabariMilele FmSwahili

Afisa mmoja wa magereza azuiliwa kwa tuhuma za kumuua mpenziwe Bomet

Polisi mjini Bomet wanamzuilia afisa mmoja wa magereza kwa tuhuma za kumuua mpenziwe katika nyumba yao mjini Bomet.

Wawili hao wanadaiwa kuzozana ambapo mshukiwa anasemekana kuchukua silaha butu na kumpiga marehemu.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Musa Imamai, marehemu aliaga dunia alipokuwa akikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Longisa.

Imamai anasema wawili hao wamekuwa na tofauti za muda mrefu, huku akiwataka wenyeji kutatua tofauti zao kwa njia mwafaka kuepuka vifo vya kiholela vinavyosababishwa na mapenzi

Show More

Related Articles