MichezoMilele FmSwahili

AFC Leopards yapigwa faini ya shilingi elfu 300 kutokana na utovu wa nidhamu

Klabu ya AFC Leopards imepigwa faini ya shilingi elfu mia tatu hii ni baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu wakati mechi ya ligi kuu taifa dhidi ya Nzoia Sugar ilichezwa tarehe 6 Januari

Kulingana na uamuzi uliotolewa na kamati ya huru ya nidhani katika kampuni ya KPL,katibu wa Ingwe Timothy Lilumbi alimdhulumu kwa mshambuliwa refa wa mechi hiyo George Mwai.

Kafuatia Uamzi huo AFC leopards ina hadi siku 30 kulipa faini hiyo ya shilingi elfu mia tatu.

Katibu Lilumbi pia hakusazwa katika hukumu hiyo na amepigwa marufuku ya miezi tano ya kutojihusisha na maswala ya soka,akilazimika pia kulipa faini ya shilingi laki tatu vilevile.

Kulingana na uamuzi huo,endapo Lilumbi ataefeli kulipa faina katika kiindi cha siku 30,klau yake itapewa msukumo wa kumgharamia.

Hadi wakati huu wa kwenda hewani hakuna ujumbe wowote ulitolewa na Leopards kuhusu maamuzi hayo,ikisalia kitendawili iwapo wataka rufaa ua watasalimu amri na kufuta maagizo.

Show More

Related Articles