HabariMilele FmSwahili

Mahakama yamwagiza afisa mkuu wa IEBC Ezra Chiloba kurejea afisini

Mahakama ya kiviwanda imemwagiza afisa mkuu wa tume ya IEBC Ezra Chiloba kurejea afisini. Jaji Stephen Radido amemtaka Chiloba kuendelea kuhudumu katika wadhfa wake huku kesi aliowasilisha kupinga uamuzi wa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kumpa likizo ya lazima ya miezi mitatu ikiendelea kusikizwa. Chebukati alimwagiza Chiloba kuondoka afisini mwezi Aprili mwaka huu kuruhusu uchunguzi wa matumizi ya kifedha zilizotengewa chaguzi za mwaka jana. Hatua ya kumtuma nyumbani Chiloba ilipelekea mgawanyiko mkubwa baina ya makamishna wa IEBC na kuwalazimu watatu kati yao kujiuzulu.

Also read:   Mhubiri Deya kujua iwapo atachiliwa kwa dhamani au la kesho
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker