HabariMilele FmSwahili

Kenya yaadhimisha siku ya kina mama ulimwenguni

Wito wa kuongeza idadi ya kina mama viongozi wa kitaifa umezidi kutolewa siku ya wanawake ikiadhimishwa leo. Mwakilishi kina mama kaunti ya Kisii Janet Ongera amewahimiza viongozi wenza wa kiume kushirikiana na wanawake katika kuwatumikia wakenya bila ubaguzi.

Gavana wa Nandi Satephen Sang akihutubia makundi ya wanawake kaunti yake amewataadharisha dhidi ya kuhujumiana wenyewe kwa wenyewe.

Also read:   Leo ni siku ya wanawake duniani

Nao wanawake katika maeneo mbali mbali wakiwemo wafungwa nchini wamepokea mafunzo kuhusu maswala mbali mbali ya kijamii na kiuchumi.

Katika ujumbe wake wa maadhimisho haya naibu rais William Ruto serikali itaendelea kuweka mikakati ya kuhimiza usawa wa jinsia kupitia kubuni sheria zinazokabili ubaguzi wa kijinsia.

Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker