Serikali yakanusha madai ya kukosa pesa za kufadhili shughuli zake

Serikali yakanusha madai ya kukosa pesa za kufadhili shughuli zake
Waziri wa fedha Henry Rotich

Serikali imekanusha madai ya kukosa pesa za kufadhili shughuli zake. Waziri wa fedha Henry Rotich anasema taarifa zilizopo nchini si kweli na zinafaa kupuuzwa. Akizungumza siku moja baada ya kuhojiwa na kamati ya seneti kuhusu fedha alikodai kenya inakabiliwa na uhaba wa fedha, Rotich anasema ilivyo sasa shughuli zote za serikali zinaendelea vyema na zimefadhiliwa na mfuko wa serikali. Kadhalika anasema shilingi bilioni 134 zimeelekezwa kwa uongozi wa kaunti 47 ikiwa ni asilimia 43 ya fedha zinazofaa kugawiwa kaunti.

Also read:   Wenyeji wa Isiolo walalamikia jinsi serikali inavyoendesha shughuli ya kuweka mipaka

Post source : Milele Fm

Related posts

MNL App
MNL App