Mwanasheria Githu Muigai ajiuzulu

Mwanasheria  Githu Muigai ajiuzulu
Mwanasheria Githu Muigai

Mwanasheria  Githu Muigai amejiuzulu. Rais Uhuru Kenyatta anasema amepokea waraka wa Muigai na hivyo kumteua jaji Paul Kihara Kariuki kuhudumu katika wadhifa huo. Muigai amehudumu kama mkuu wa sheria kwa muda wa miaka 6 sasa. Wakati huo huo rais Kenyatta amemteua Kenedy Ogeto kuhudumu kama mkuu wa sheria huku Njee Muturi aliyeshikilia wadhifa huo akiteuliwa kama naibu mkuu wa wafanyikazi serikalini. Aidha rais amependekeza wakili Abdikadir Mohammed kuhudumu kama balozi wa Kenya Korea Kusini. Hadi leo wakili Abdikadir amehudumu kama mshauri wa rais Kenyatta katika maswala ya sheria na amekuwa akihudumu katika ikulu ya Nairobi

Also read:   Rais kuongoza hafla ya kufuzu kwa maafisa 3985 wapya wa polisi

Post source : Milele fm

Related posts

MNL App
MNL App