Peter Kenneth kuwania ugavana Nairobi kama mgombea huru

Peter Kenneth kuwania ugavana Nairobi kama mgombea huru
Photo: peter Kenneth

Peter Kenneth atawania ugavana kaunti ya Nairobi kama mgombea huru. Kenneth anasema amechukua uamzi huo baada ya kushauriana na wafuasi wake. Katika kikao na wanahabari hapa Nairobi, Kenneth anasema yuko tayari kukabiliana wapinzani wake. Kenneth ambaye alishindwa katika uteuzi wa mchujo wa Jubilee na seneta Mike Sonko amedai uteuzi huo ulikumbwa na dosari nyingi na hawezi kukubali matokeo yake. Hata hivyo amesema anamuunga mkono rais Uhuru Kenyatta.

Also read:   Nairobi Governor Evans Kidero, Peter Kenneth face off at ACK church

Post source : Milele fm

Related stories