Raila azungumzia vurugu zilizoshuhudiwa katika mchujo wa ODM

Raila azungumzia vurugu zilizoshuhudiwa katika mchujo wa ODM
Photo: Raila Odinga

Kwa mara ya kwanza kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amezungumzia ghasia zilizokumba mchujo wa chama hicho akiondolea lawama bodi ya uchaguzi wa chama. Akizungumza baada ya kukutana na wagombea wa viti mbalimbali kupitia chama hicho hapa Nairobi Raila amesema ODM ilikuwa imejiandaa vilivyo kwa mchujo lakini ubinafsi wa baadhi ya wagobmea ndio ulisababisha kuwsambaratika zoezi hilo maeneo kadhaa.

Also read:   Wanaume watafuta wajane matajiri na kuwadhulumu, Nyatike

Aidha amesema ODM ilikuwa na wagombea wengi kaitka viti mbalimbali na juhudi za chama kujaribu kutumia maelewano hazikufua dafu hivyo kupelekea baadhi yao kutumia majambazi kusambaratisha mchujo.

Wakati huo huo kinara wa wiper Kalonzo Musyoka naye anakutana na makundi ya wasomi, viongozi na wazee kutoka jamii ya ukambani kupanga mikakati ya kuimarisha chama hicho uhaguzi ukikaribia.

Also read:   Raila: Kalonzo yuko ndani ya NASA na tuko imara

Post source : Milele Fm

Related stories