Seneta Kuti ajiunga na NARC Kenya

Seneta Kuti ajiunga na NARC Kenya
Photo: Milele Fm

Seneta wa Isioli Mohammed Kuti amejiunga na chama cha NARC Kenya siku moja baada ya kujiuzulu kama mwanachama wa Jubilee. Kuti anayewania ugavana Isiolo, amedokeza kukosa imani na bodi ya uchaguzi ya Jubilee kaunti ya Isiolo anayosema imedhihirisha kuwapendelea baadhi ya wawaniaji katika kinyanganyiro cha ugavana kaunti hiyo. Hata hivyo amesema bado anamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena katika uchaguzi mkuu ujao.

Also read:   Rais hampendelei mgombea yeyote katika kinyanganyiro cha ugavana Nairobi

Post source : Milele Fm

Related stories