Mazungumzo yakusitisha mgomo wa madaktari yang’oa nanga

Mazungumzo yakusitisha mgomo wa madaktari yang’oa nanga
Photo: Milele Fm

Mazungumzo ya kusitisha mgomo wa madaktari  yameng’oa nanga leo chini ya usukani wa tume ya kitaifa ya haki za kibinadamu KNHCR na chama cha wanasheria LSK.Mazungumzo hayo ambayo yamesalia kuwa siri kwa wahusika hadi pale suluhu litapatikana yanafanyika katika afisi za KNHCR hapa jijini Nairobi.Taarifa kuhusu kilichojiri katika mazungumzo hayo yanayohusisha tume ya KNHCR, chama cha LSK, muungano wa madkatari KMPDU, wizara ya afya na baraza la magavana zimesalia finyu kwani hakuna ripoti kamili hadi pale kutakapopatikana maafikiano.mwenyekiti wa KMPDU Samuel Oroko anasema kutokana na wao kufungwa sasa wana nafasi ya kuamua jinsi mazungumzo hayo yatafanyika na pia kuamua hatima ya mgomo wao uliodumu kwa siku 75 sasa.

Also read:   Ukatili wa polisi: Boinnet atakiwa kumchukulia OCPD wa Kayole hatua

Post source : Milele Fm

Related stories