Madaktari wapewa makataa ya wiki mbili kusitisha mgomo

Madaktari wapewa makataa ya wiki mbili kusitisha mgomo
milele fm

Wakuu wa muungano wa madaktari KMPDU wamepewa makataa ya wiki mbili kusitisha mgomo unaoendelea. Akitoa uamuzi huo jaji wa mahakama ya viwanda Hellen Wasilwa amesema watahukumiwa kifungo cha mwezi mmoja iwapo watakaidi agizo hilio. Wasilwa pia amewataka kukoma kudai mishahara kwa misingi ya mkataba uliotiwa saini na serikali mwaka 2013 akisema mkataba huo si halali. Viongozi hao walikuwa wameitaka mahakama kutowapa adhabu kali wakidai huenda ikaathiri mazungumzo yanayoendelea kutatua mgomo huo.

Also read:   Juhudi za kumaliza mgomo wa madaktari wagonga mwamba

Post source : milele fm

Related posts

MNL App
MNL App