Mchujo wa Jubilee wafutiliwa mbali katika kaunti 11

Mchujo wa Jubilee wafutiliwa mbali katika kaunti 11

Chama cha Jubilee kimeahirisha uteuzi wake wa mchujo katika kaunti 11 nchini.

Katibu mkuu Raphael Tuju anasema hatua hiyo imechukuliwa baada ya mashauriano ya kina na rais Uhuru Kenyatta na kutathimini hali ilivyokua katika kaunti hizo.

Aidha amewalaumu baadhi ya maafisa wa chama hicho waliofaa kuendesha zoezi zima la mchujo kwa kuathiri shughuli kutokana na kile kilichotajwa kama ukatili kwa chama akisema hatua kabambe zitachukuliwa dhidi ya wahusika.

Also read:   Kenya yaponea marufuku ya kutoshiriki michezo ya Olimpiki kufuatia shoka la WADA

Related stories