Mudavadi: ANC kufanya uteuzi kivyake kaunti 37

Mudavadi: ANC kufanya uteuzi kivyake kaunti 37

Ndoto ya vyama tanzu vya muungano wa upinzani NASA ya kufanya chaguzi za pamoja za mchujo katika baadhi ya maeneo humu nchini na hasw jijini Nairobi, imeonekana kuyumba yumba zaidi, baada ya chama cha ANC, kinachoongozwa na Musalia Mudavadi, kutangaza kwamba kitaandaa chaguzi zake za mchujo kuanzia tarehe tatu mwezi ujao katika kaunti thelathini na saba kati ya 47 kote nchini.
Juma lililopita, gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero, alinukuliwa akidai kwamba muungano wa NASA tayari umeafikiana kuandaa mchujo wa pamoja katika kaunti ya Nairobi katika viti vyote vya kisiasa.
Hata hivyo msimamo wa kuwepo kwa zoezi la mchujo wa pamoja umepingwa vikali na baadhi ya viongozi wa muungano huo.

Also read:   Wakaazi wajeruhiwa na mabomu ya wanajeshi wanaofanya mazoezi katika kambi, kaunti ya Isiolo

Related stories