MIHEMKO YA KAUNTI : Kinyang’anyiro cha ugavana kaunti ya Wajir

MIHEMKO YA KAUNTI : Kinyang’anyiro cha ugavana kaunti ya Wajir

Joto la kisiasa katika kaunti ya Wajir linaonekana kupamba moto kila kuchao.
Tayari mahasimu wakuu wa kisiasa gavana wa sasa Ahmed Abdullahi pamoja na aliyekuwa balozi wa Kenya nchini Saudia Mohammed Mahmud wamepata ridhaa mabaraza tofauti ya wazee kutoka jamii ya Degodia.
Kulingana na wenyeji wa kaunti ya Wajir, mbali na ukoo kuchangia pakubwa watakayemuunga mkono, watatathmini utendakazi wa mhusika akihudumu kabla kumhukumu.
Kwenye Mihemko ya Kaunti wiki hii, Caleb Ratemo amerejea kutoka kaunti ya Wajir ambapo kuna koo tatu kuu Ajuran, Degodia na Ogaden ambazo zinatawala siasa za kaunti hiyo pana.

Also read:   Mihemko ya Kaunti: Kaunti ya Migori

Related stories