HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Wasiotambulika: Tunamuangazia mkaazi wa Elgeyo Marakwet anayekabili pombe haramu

Miaka mitatu iliyopita shirika la kupambana na mihadarati na pombe nchini, NACADA liliorodhesha kaunti ya Elgeyo Marakwet kama moja wapo wa maeneo yaliyoathirika na utengenezaji wa pombe haramu nchini.

Mwanamume mmoja kutoka eneo hilo Samuel Teimuge alikerwa sana na taarifa hiyo akaamua kuwatafuta wagema haswa kina mama na kuwarai kujiunga na mradi wa kurekebisha tabia uliolenga kuwafungua macho kuanzisha njia mbadala za kujitafutia riziki.

Hii leo, Teimuge, amewarekebisha kina mama 1,200 ambao sasa ni wakulima hodari.

Show More

Related Articles