HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Kivangaito cha Embakasi: Makataa ya Rais ya miezi 3 yakamilika bila suluhu kupatikana

Licha ya Rais Uhuru Kenyatta kutoa makataa ya miezi mitatu kwa usimamizi wa kampuni ya Embakasi Ranch kumaliza zogo linalokumba kampuni hiyo la uuzaji wa mashamba hewa, imebainika kuwa agizo hilo la rais halitatimika katika kipindi hicho jinsi alivyotaka.

Hata hivyo, ni wazi kuwa kumaliza zogo la ardhi hiyo ni mtihani mkubwa huku wanahisa waanzilishi wanaodai kuimiliki radhi husika, wakisema wanachezwa shere na kampuni tajika katika juhudi za kupata uhakiki wa ni nani wanaomiliki kipande hicho cha ardhi.

Je? kunani Embakasi? tupate makala maalum ya Kivangaito Cha Embakasi sehemu ya pili naye Franklin Wallah kwa uwazi na undani wa mambo katika jitihada za kutegua kitendawili cha ardhi hiyo jinsi alivyotaka Rais Uhuru Kenyatta.

Show More

Related Articles