
Dawa za kukabiliana na bakteria mwilini zimetumika miaka nenda miaka rudi.
Lakini sasa madaktari wanaonya kwamba upungufu wa makali ya dawa hizo kukabiliana na maradhi mwilini unayumbisha juhudi za kukabiliana na maradhi.
Hali hii imechangiwa pakubwa na matumizi mabaya ya dawa hizo bila ya maagizo ya daktari.