Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

NCCK yapendekeza mabadiliko kurejesha wadhifa wa Waziri Mkuu

Baraza la makanisa nchini, NCCK limemtaka mkenya yeyote au shirika lolote linalopania kupinga ushindi wa rais mteule Uhuru Kenyatta na naibu rais mteule William Ruto, kuwasilisha ombi lake mbele ya mahakama ya upeo na kufuata mkondo wa sheria na katiba, bila ya kulitumbukiza taifa kwenye mtafaruku wa kikatiba na kuligawanya taifa.
Tayari mwanaharakati Okiya Omtata ashawasilisha ombi lake litakalosikizwa novemba tarehe kumi huku muungano wa makanisa vile vile ukipendekeza kuwa baada ya joto la kisiasa kutulia basi katiba ifanyiwe marekebisho na nyadhifa za waziri mkuu na manaibu wake wawili pamoja na kiongozi rasmi wa upinzani na naibu wake kuorodheshwa.

Show More

Related Articles