Wauguzi washtumu SRC kwa kulemaza juhudi za kutatua mgomo

Wauguzi washtumu SRC kwa kulemaza juhudi za kutatua mgomo

Huduma za matibabu katika hospitali za umma zinaendelea kuathiriwa na mgomo wa wauguzi ambao umeingia wiki ya tatu hii leo kwa maandamano, huku wauguzi wakishikilia kuwa hawatarejea kazini hadi matakwa yao yatakapotimizwa.
Wauguzi hao walianza maandamano yao katika Bustani ya Uhuru  kabla ya kuandamana hadi katika afisi za serikali tofauti ikijumuisha afisi za tume ya kuratibu mishahara ya SRC, pamoja na afisi za Wizara ya Afya  kuwasilisha matakwa yao.
Hata hivyo hawakuhutubiwa na yeyote kutoka afisi hizi.
Wauguzi hao wameishutumu tume ya SRC kwa kulemaza shughuli ya kutiwa saini kwa mkataba wao wa kurejea kazini.

Also read:   Kura za ugavana kuhesabiwa upya katika kaunti ya Homabay

Related posts

MNL App
MNL App